12 Juni 2024 - 15:59
Mtoto wa rais wa Marekani Joe Biden apatikana na hatia kwenye kesi tatu

Mtoto wa rais wa Marekani amepatikana na hatia katika kesi zote tatu zilizokuwa zinamkabili ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kununua silaha wakati akiwa mtumiaji wa dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Hunter Biden, mtoto wa kiume wa rais wa Marekani Joe Biden mwenye umri wa miaka 54, alihukumiwa jana Jumanne na mahakama ya majaji 12 huko Wilmington, Delaware, na kumpata na hatia ya kusema uwongo kuhusu matumizi yake ya dawa za kulevya kwa ajili ya kununua silaha kinyume cha sheria.
Hunter Biden alishtakiwa kwa kutoa taarifa mbili za uwongo wakati wa kujaza fomu ya kununua bastola aina ya Colt mwezi Oktoba 2018; kwanza kwa kusema uongo kwamba hakuwa mraibu wa dawa za kulevya, na kisha kwa kutangaza taarifa hiyo kuwa ni kweli na tatu kwa ni kumiliki silaha kinyume cha sheria kwa siku 11, kabla ya hawara wake, Hallie Biden, kuitupa kwenye pipa la taka kwa hofu. Gazeti la The Fuardian limeandika kuwa, baada ya kuvunjika ndoa yake, Hunter Biden alianzisha uhusiano wa kimapenzi na Hallie Biden, ambaye alikiri kuvuta madawa ya kulevya aina ya crack pamoja na Hunter Biden. Wakili maalumu, David Weiss alimshtaki Hunter Biden kwa uhalifu unaohusiana na kutoa taarifa za uwongo wakati akinunua silaha mwaka 2018, ambavyo waendesha mashtaka wanadai alikuwa nayo wakati anatumia dawa za kulevya.

342/